Maafisa wa usalama Nigeria wamesema kuwa zaidi ya wanawake
60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo wamewatoroka wanamgambo wa Boko Haram
waliokuwa wamewateka nyara.
Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68
waliotekwa mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa kaskazni mashariki mwa jimbo
la Borno.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda
wasichana hao walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda
kushambulia kambi ya kijeshi.
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa Ijumaa hiyo
walifanikiwa kuwaua wapiganaji zaidi ya 50 karibu na mji wa Damboa.
Hata hivyo bado wanamgambo hao wa Boko Haram wanawashikilia
zaidi ya wasichana wengine 200 waliowateka nyara mwezi Aprili.

